Friday, 23 August 2013

Wahamiaji haramu waitikisa Mbeya


 
Na Godfrey Kahango  (email the author)

Posted  Alhamisi,Agosti22  2013  saa 20:43 PM
Kwa ufupi
Hata hivyo imebainika kuwa Mkazi wa Tunduma Oden Said (28) amekuwa akihusika na biashara usafirishaji wa raia 28 wa Ethiopia, baada ya taarifa ya Polisi Mkoa wa Mbeya kueleza kuwakamata wahamiaji hao.


Mbeya. Wimbi la wahamiaji haramu limezidi kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya wahamiaji hao kutoka nchi mbalimbali hususan Ethiopia kuendelea kuingia katika mkoa huo bila kibali licha ya vyombo vya dola kuwatia mbaroni mara kwa mara.
Hata hivyo imebainika kuwa Mkazi wa Tunduma Oden Said (28) amekuwa akihusika na biashara usafirishaji wa raia 28 wa Ethiopia, baada ya taarifa ya Polisi Mkoa wa Mbeya kueleza kuwakamata wahamiaji hao.
Kamanda wa Polisi Mbeya, Diwani Athuman alisema Chenet Jabamo na wenzake 27 walifanikiwa kuingia nchini kinyume cha sheria za uhamiaji za nchi huku akibainisha kwamba polisi wanamshikilia mkazi huyo wa Tunduma kwa tuhuma za kuhusika na kuwasafirisha raia hao kwa njia ya kificho.