Kwa ufupi
Mangula alisema alifanikiwa kubadilisha nguo
wakati akielekea kwenye ukumbi huo waligongana uso kwa uso na gari aina
ya Spacio na kumsababishia maumivu ambapo aliwahishwa Hospitali ya Aga
Khan.
Dar es Salaam. Mazishi ya mtoto wa Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Nemela yanatarajiwa kufanyika
leo katika Kijiji cha Kinenulo mkoani Njombe.
Akizungumza juzi nyumbani kwake Osterbay
walipokuwa wakiuaga mwili wa marehemu, Mangula alisema mwili huo
unasafirishwa hadi kijijini kwao ambapo wanatarajia kuzika leo saa 10
jioni.
Mangula alisema Nemsela alipata ajali Agosti 15
mwaka huu eneo la Hospitali ya Aga Khan akitokea kwenye sherehe ya
kumuaga bibi harusi ambaye alikuwa anaolewa na kaka yake.
Alisema sherehe hiyo ilifanyika Agosti 15, mwaka
huu kwenye Ukumbi wa Water Front na ilipofika saa 3.00 usiku alilazimika
kwenda nyumbani kubadili nguo yake baada ya kuchanika ghafla. Alipokuwa
akirudi alipata ajali na alifariki siku ya harusi Agosti 17.
chuwaambapo Nemela alikuwa anacheza muziki mara
nguo yake ilichanika na alilazimika kumchukua rafiki yake wakapanda gari
lake aina ya Toyota Starlet kwa ajili ya safari ya kuelekea nyumbani
kubadilisha nguo.
Mangula alisema alifanikiwa kubadilisha nguo
wakati akielekea kwenye ukumbi huo waligongana uso kwa uso na gari aina
ya Spacio na kumsababishia maumivu ambapo aliwahishwa Hospitali ya Aga
Khan.
“Tulikuwa wote ukubini kwenye sherehe ya kumwaga
mke wa mtoto wangu wa kiume ambayo ilifanyika Ukumbi wa Water
Front,ilipofika saa 3 usiku wakati akiwa anacheza nguo yake ilichanika
na kulazimika kwenda nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo,”alisema
Mangula.
Alisema alifanyiwa uchunguzi hospitalini hapo na
baadaye waliambiwa waende Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
Mangula alisema saa 7 usiku walimpeleka katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alitibiwa na kuruhusiwa nyumbani
Agosti 16, mwaka huu.
Alisema Agosti 16 mwaka huu saa 8 usiku Nemela
alianza kutapika hivyo walilazimika kumpeleka Hospitali ya Muhimbili kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
Alisema Agosti 17 mwaka huu baada ya uchunguzi
iligundulika kuwa damu ilikuwa inatoka ndani ya ini hivyo daktari
walilazimika kumfanyia upasuaji saa 8 mchana.
“Siku hiyo sitaisahau ilikuwa ni ya matukio mawili
ya watoto wangu , marehemu Nemela na kaka yake Malumbo ambaye alikuwa
anafunga ndoa muda wa saa 10 jioni ambayo mwanagu aliaga dunia,”alisema
Mangula.