Waziri
wa ujenzi Mh Dk John Magufuli amewataka makandarasi wote
waliosajiliwa kuhakikisha kuwa ndani ya mwaka mmoja wote wawe wamekula
kiapo cha kiukandarasi mahakamani na kuagiza kuwa wale wote ambao
watakaidi agizo hilo wasipewe kazi na kuwataka watambue kuwa taifa
kwanza mambo mengine baadaye .
Mh
Maguli ameyasema hapo alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa
makandarasi ambapo amesema kazi ya kikandarasi ni kazi ya kiadilifu na
hivyo ni lazima makanadatasi wote wajiepushe na vitendo vya rushwa kwa
faida ya taifa
Aidha
kwa upande wawakanadarasi walioshiriki katika mkutano huo akiwemo
mhandisi mathias mwambona na mhandisi Andrew Ndalilo wamebainisha
mambo mbalimbali katika tasnia hiyo huku wakiiomba serikali kuona
namna nzuri zaidi ya kuwajengea uwezo wakandarsi wa ndani.
Katika
mkutano huo pia baadhia ya wahandishi walikula kiapo mbele ya hakimu
kutoka katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu pamoja na baadhia ya
wanafunzi wa kike waliofanya vyema katika masomo yao ya sayansi katika
vyuo vikuu mbalimbali akiwemo Golder Kamuzora kutoka chuko kikuu cha
Dar es salaam.
source: ITV-Daima