Absalom Kibanda
 Mhariri Mkuu wa gazeti la Mtanzania aliyenusurika kuwawa baada ya 
kuteswa kwa kung'olewa kucha, meno, jicho na vidole sasa anakuwa hana 
kazi kwa miezi 3 baada ya gazeti lake kufungiwa na Serikali. Wamemkosa 
kwa kumtesa sasa wanafuata kwenye kazi yake. Hawataki kumwua Kibanda kwa
 njaa, wanataka kuwanyima habari Watanzania. Wanataka tusome Uhuru na HabariLeo tu. 
 Unafungia gazeti la mwananchi eti kwa kuandika kuhusu mishahara ya  
Serikali, wapuuzi hawa hawajui mishahara ni kodi za wananchi na wana 
nchi wana haki ya kujua mishahara ya watumishi wao. Serikali lazima 
ijutie uamuzi huu wa kibabe na kidikteta. Kama hupendi habari ya gazeti 
nenda mahakamani. Kufungia gazeti ni tendo la woga. Cowards behave this 
way
