Sunday 29 September 2013

Salma Kikwete azuru Jimbo la Nebraska, Marekani


SATURDAY, SEPTEMBER 28, 2013


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe Ricketts kwenye uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens, 7, mara baada ya Mama Salma kutua kwenye uwanja wa ndege wa Omaha katika jimbo la Nebraska nchini Marekani. Kwa picha zaidi na John Lukuwi BOFYA HAPA






Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyeshwa na Bwana James Ricketts, Rais na Mtendaji Mkuu wa wa Taasisi ya Oppoturnity Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya elimu kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi hiyo yenye Makao Makuu yake huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Opportunity Education iliyoko huko Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo kwa kutambua mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake ya WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina mama..

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Taasisi ya Opportunies Education kwenye ofisi za taasisi hiyo huko Omaha Nebraska nchini Marekani. Kulia kwake ni katubu wa WAMA Bw. Daudi Nasibu

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Mshauri Mwandamizi wa United Nations Fund for International Partnership (UNFIP)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akwia kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Mshauri Mwandamizi wa United Nations Fund for International Partnership (UNFIP)

.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Dr. Marjorie Kastelnik, Dean, College of Education and Human Sciences kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska ambapo Mama Salma alishiriki kwenye Gala to support Global Education kwenye Chuo Kikuu cha Lincoln huko Nebraska

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Bwana Joe Ricketts kwenye hafla ya Taasisi ya Support Global Education .

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa waliohudhuria hafla ya Taasisi ya Support Global Education iliyoandaliwa kwa ajili ya kumtunuku tuzo maalum Bwana Joe Ricketts kwa juhudi zake za kuboresha elimu duniani hasa katika nchi zinazoendelea.

PICHA NA JOHN LUKUWI

SOURCE: JAMII FORUM