Sunday 29 September 2013

Malalamiko ya Wanepali nchini Qatar yanaoana na ya Mtanzania Abdul nchini Yemen

  28/09/2013 
 Picture

 (picha: The Guardian)


Yanayosimuliwa kwenye video iliyopachikwa hapo chini na raia wa Nepal kuhusu maisha ya wanayolazimika kuishi Qatar baada ya kulipwa ujira mdogo na kunyang'anywa pasipoti zao, yananikumbusha Matanzania, Abdul alivyosimulia (unaweza kubofya hapa kusikiliza) yaliyomsibu baada ya kuahidiwa kazi yenye malipo manono na marupurupu ya kutosha, kabla ya kufika Yemen, kunyang'anywa pasispoti, kutokupata msaada kutoka kwenye vyombo vya usalama na sheria vya nchi hiyo na kutishiwa uhai wake na familia yake. 

Source: http://www.wavuti.com