Na James Magai, Mwananchi (email the author)
Posted Jumatano,Julai10 2013 saa 14:14 PM
Kwa ufupi.
Dar es Salaam. Kesi ya Ugaidi inayowakabili makada watano Chadema katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetua Mahakama Kuu.
Washtakiwa hao kupitia kwa mawakili wao
wanaowatetea, Peter Kibatala na Profesa Abdallah Safari, wamewasilisha
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Tabora, kuwa haina uwezo wa kusikiliza maombi yao.
Washtakiwa hao katika kesi hiyo inayosikilizwa na
Hakimu Mkazi Joctan Rushwera, ni Katibu wa Chadema Wilaya ya Kinondoni,
Dar es Salaam.
Wengine ni Henry John Kilewo, Evodius Justinian,
Oscar Kaijage, Rajab Daniel, Seif Magesa Kabuta, wote ni makada wa
Chadema kutoka mikoa mbalimbali.
Wote wanakabiliwa na mashtaka mawili, moja la kumteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora.
Shtaka la pili ni kumdhuru Tesha kwa kumwagia Tindikali.
Wakili Kibatala alimweleza mwandishi wa habari
hizi jana, kuwa hawakubaliani nao kwani wanaamini ina uwezo wa kutoa
uamuzi maombi yao.
“Tunaamini kuwa mahakama ina uwezo huo, ndiyo
maana tulitoa hoja zetu na upande wa mashtaka nao ukajibu na hakimu
akarekodi,” alisema.
Kesi inatarajiwa kutajwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora Julai 22, mwaka huu.