Wednesday 24 July 2013

Tanzania katika skendo ya Matumizi mabaya ya pesa za misaada kutoka Norway



 Na Dk



Katika gazeti maarufu hapa Norway almaarufu kama "Aftenposten" ambalo usomwa na watu wengi nchini hapa katika ukurasa wake wa kwanza limetoa picha ya "Mafia Island" ambacho ni kisiwa mmoja wapo cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kichwa cha habari cha gazeti hilo kilikuwa " Errors have been detected in other ocean aid case"

Katika makala hiyo, Mwandishi wa gazeti hilo anaielezea ripoti maalumu kutoka Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Norway jinsi Tanzania ilivyo tafutana takribani krona milion 150kati  ambazo ni sawa na bilioni 4.8 za Tanzania.
Pesa hizo ni sehemu ya ufadhili wa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara na mazingira huko Mafia. Kutokana na kichwa cha habari ni dhahiri kuwa serikali ya Norway inahituhumu Tanzania kwa matumizi mabaya ya pesa yao ya walipa kodi wao katika miradi inayoifadhili nchini Tanzania. Na hii si mara ya kwanza kwa report ya namna hii kutoka.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeorodheshwa kama wafujaji wa pesa za maendeleo. Nchi nyingine ni Afghanistan ambayo imeripotiwa kutumia pesa vibaya takribani krona milion 35.


Gazeti hilo limedokeza kuwa cha kushangaza ni kwamba si ajabu atua zozote zisichukuliwe juu ya watu wote waliohusika katika ubadhilifu huo wa pesa zao.








Taarifa hii itaendelea hapo baadae.