Kwa ufupi
Rais Jakaya Kikwete tayari amemtumia salamu
Rais Omar al-Bashir kufanya uchunguzi na kuhakikisha wote waliohusika na
mauaji hayo wanachukuliwa hatua kali.
Dar es Salaam na Mashirika.
Wakati miili ya askari waliouawa Darfur ikiagwa leo kwenye Viwanj a vya
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga Dar es Salaam, Mwendesha Mashtaka wa
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Fatou Bensouda ametoa tamko kali
dhidi ya mauaji hayo.
Katika taarifa yake aliyoitoa juzi, Bensouda
alimwomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Ban Ki-moon na wadau
wengine wote ndani ya UN pamoja na Jumuiya za Kimataifa kufanya
uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo na kuwachukulia hatua wale wote
waliohusika.
Rais Jakaya Kikwete tayari amemtumia salamu Rais
Omar al-Bashir kufanya uchunguzi na kuhakikisha wote waliohusika na
mauaji hayo wanachukuliwa hatua kali.
Habari zilizopatikana juzi zilidai kuwa askari
hao wa kulinda amani waliuawa na kundi la wanamgambo wanaoungwa mkono
na Kundi la Janjaweed.
Waagwa leo
Wapiganaji hao saba wa Tanzania waliuawa walipokuwa wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na Afrika, Darfur, UNAMID.
Askari hao wanaagwa leo kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Upanga, Dar es Salaam.
Kaimu Msemaji wa JWTZ, Meja Joseph Masanja
aliiambia Mwananchi jana kuwa Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri
Jeshi Mkuu wa Tanzania, ni miongoni mwa mamia ya waombolezaji
wanaotarajiwa kutoa heshima za mwisho kwa wapiganaji hao waliouawa Julai
13, kwenye mji, Darfur.
Source: Mwananchi news paper
Source: Mwananchi news paper