Kwa ufupi
kuongeza: “Hivi sasa uchunguzi unaendelea,
lakini hatuwezi kuwa kila siku ni uchunguzi tu na wakati mwingine
uchunguzi umekuwa hauna matokeo.”
kuongeza: “Hivi sasa uchunguzi unaendelea,
lakini hatuwezi kuwa kila siku ni uchunguzi tu na wakati mwingine
uchunguzi umekuwa hauna matokeo.”
Alisema watumishi kama hao hawafai kwa kuwa wanatumia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha wao binafsi.
Mkutano wa Smart Partnership Dialogue ulifanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 28 hadi Julai Mosi mwaka huu.
Alisema walifahamu kuhusu ufisadi huo baada ya
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kueleza kuwa kuna utata kwenye fedha
hizo na kwamba kampuni tatu hewa zililipwa fedha wakati hazijasajiliwa
kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).
“Kuna kampuni kama tatu, hizi nasikia
zimeshachukuliwa hatua kwa kuwa ni hewa lakini bado... lazima CAG afanye
ukaguzi kwa hizo Sh8 bilioni,” alisema Sitta.
Sitta ambaye amekuwa akijipambanua kuwa ni mmoja
wa kundi la viongozi wanaopinga ufisadi, alisema watumishi wa jinsi
hiyo, hawafai kwa kuwa wanatumia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha
binafsi.
“Pamoja na yote, kampuni zina watu, lazima na wao
wachukuliwe hatua. Wahusika wote ninaamini wanafahamika sasa isifikie
hatua tunaambiwa uchunguzi usiofikia mwisho,” alisema Sitta.
Hata hivyo, Balozi Sefue hakupatikana jana
kuelezea tuhuma hizo ambazo hivi karibuni ziliripotiwa na gazeti moja la
kila wiki kwani simu yake iliita bila ya majibu na hata alipotumiwa
ujumbe mfupi hakujibu na baadaye simu yake haikuwa tena hewani.
Aendelea kuponda Serikali Tatu
Sitta aliendelea na msimamo wake wa kupinga
mapendekezo ya Tanzania kuwa na Serikali Tatu akisema wanaopigania hilo
wana masilahi binafsi.
Sitta ambaye aliwahi pia kuwa Spika wa Bunge,
alishawahi kutoa msimamo wake kuhusu Serikali Tatu kama
zilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Rasimu ya
Katiba akisema hakuna nchi duniani yenye utawala wa marais watatu na
endapo Tanzania itakuwa hivyo, itaweka rekodi ya kuwa ya kwanza.
Sitta ambaye mara kadhaa ametajwa kuwa miongoni
mwa wanasiasa wanaotaka kuwania urais mwaka 2015, alisema Katiba ina
masilahi ya watu aina mbalimbali lakini hatari anayoiona ni kwa wale
wenye masilahi binafsi ambao wanaweza kuathiri mchakato huo kwa kuwa
wanafikiria urais.
“Tunaweza kuwa na Serikali Tatu bila kuwa na marais watatu.
Tukiwa na Serikali Tatu tuwe na rais mmoja na labda naibu rais au makamu
wa rais au waziri mkuu, haiwezekani tukawa na marais watatu kwani hiyo
ni gharama kubwa,” alisema. “Kuna wakati nilisema hiki ni kioja fikiria
rais anasafiri kwenda nje halafu unasikia huyu ni wa Tanganyika huyu ni
wa Muungano na huyu ni wa Zanzibar hata watu watatushangaa.”
Aidha, Sitta aliwaambia vijana hao kuwa hakubaliani na pendekezo la kuwa na mawaziri 15 katika Serikali ya Muungano.
“Utakuwaje na mawaziri 15 na wabunge wengi
kujadili mambo saba ya Muungano? Kwa nini tusiwe na mawaziri saba kwa
ajili ya kusimamia mambo hayo?”
Alisema ni vyema vijana wakajadili hayo mambo kwa
kuwa ni wao watakaonufaika au kinyume chake na Katiba Mpya kwani takwimu
zinaonyesha kwamba walio na umri wa chini ya miaka 35 nchini ni
asilimia 70.
Waziri Sitta alisema vijana wanahitaji kuwezeshwa
zaidi kwa kuwa mchakato wa Katiba Mpya bado ni mrefu na wao ndio
wanatakiwa kufaidika nao.
Alisema baadhi ya viongozi wa kijamii na kisiasa
ambao ni walafi wamekuwa wakiwanunua kwa masilahi yao binafsi... “Vijana
wa Tanzania ni baridi sana kwani baadhi yenu mnakubali kununuliwa kitu
ambacho ni hatari kwa kuwa mnakaribisha Tanzania isiyotawalika.”
“Haiwezekani nchi ina wenye uwezo kupita kiasi huku wengine wakiwa
hohehahe, lazima vijana muwe wanaharakati wa kupigania utawala bora na
kuiepusha nchi isije ikaingia kwenye matatizo ya kutokuwa na amani.”
chanzo: Mwnanachi news paper
chanzo: Mwnanachi news paper