“Na ninyi wakandarasi acheni sababu , kamilisheni  ujenzi wa barabara hizi.”
Dk John Magufuli 
            
Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi,Dk John Magufuli amewaagiza makandarasi kuendelea na kazi za ujenzi wa barabara hata kama watu watakimbilia mahakamani kufungua kesi kwa sababu miradi mingi imekuwa ikicheleweshwa kwa kigezo hicho.
  Dk Magufuli alitoa agizo hilo jana baada ya 
kukagua miradi ikiwamo barabara zinazopanuliwa kwa ajili ya kupunguza 
msongamano, Daraja la Kigamboni na mradi wa mabasi yaendayo kasi.
  Alisema baadhi ya watu wamejenga kwenye hifadhi 
ya barabara na pindi wanapoona zinataka kupanuliwa wamekuwa wakikimbilia
 mahakamani na kusababisha miradi mingi kuchelewa kukamilika kwa 
wakati.  “Msongamano unatuletea matatizo makubwa hadi ndoa nyingine 
zinavunjika hivyo tutoe ushirikiano ,” alisema Magufuli.