Kwa ufupi
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema
kauli ya Mbowe inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake
kufundishwa kumlinda yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko
hizo.
Moshi. Mwanasiasa mkongwe
nchini, Peter Kisumo, amemvaa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman
Mbowe akimtaka aache kile alichodai ni kuitumbukiza nchi kwenye
machafuko.
“Unaposema huna imani na JWTZ, huna imani na
Polisi wetu unataka kuanzisha vikundi vya kukulinda tafsiri yake ni
kwamba unataka kuanzisha vikundi vyenye sare hii si sahihi,” alisema.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema
kauli ya Mbowe inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake
kufundishwa kumlinda yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko
hizo.
“Zipo nchi zina mapesa mengi na zipo tayari
kufadhili machafuko nchi nyingine lakini nchi zilizostaarabika kama
Ujerumani, Marekani, Uingereza na nyingine haziwezi kujiingiza huko,”
alisema.
Alisema anaamini hata
Ujerumani ambayo imekuwa ikikifadhili Chadema, haitakubali kutoa fedha
kufadhili uanzishwaji wa vikundi hivyo vya ulinzi wakati vyombo halali
vya ulinzi ni Polisi na JWTZ.
Kisumo alifafanua kuwa vyama vya siasa vina sare
zake na kusema CCM, Chadema na Cuf navyo vina sare lakini kutaka
kuanzisha vikundi vya ulinzi inamaanisha vitapaswa kuwa na sare za
kijeshi.
Kwa mujibu wa Kisumo, anaamini vyombo vya ulinzi
na usalama nchini havitaruhusu kutekelezwa kwa mpango huo kwani
unalenga kuwachochea wafuasi wa Chadema kutokutii mamlaka ya dola.
Suala la Chadema kutangaza mpango wake wa
kuanzisha vikundi vya ulinzi limeibua mjadala mkali kati yake na CCM
ambacho kinamiliki kikundi cha Green Guard huku Chadema wakimiliki Red
Brigad