Posted Alhamisi,Julai18 2013 saa 22:46 PM
Kwa ufupi
Ilipangwa kujenga tanki lenye uwezo wa
kuhifadhi maji lita 135,000, lakini mkandarasi aliamua kujenga tangi
lenye uwezo wa kuhifadhi lita 90,000 ili kuuunganisha na tanki la zamani
lenye uwezo huohuo lakini mkandarasi hakuunganisha matanki hayo jambo
ambalo ni kosa’’ alisema..
Tanga. Katika hatua inayoashiria kuchoshwa na utekelezaji usioridhisha wa miradi, Mbunge wa Jimbo
la Bumbuli, wilayani Lushoto, January Makamba amekataa kuupokea mradi
wa maji uliojengwa katika Halmashauri Mpya ya Bumbuli kutokana na kile
alichokieleza kuwa umejengwa chini ya kiwango.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Bumbuli, Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia alisema kuwa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh400
milioni haukutekelezwa ipasavyo pamoja na kutengewa fedha nyingi na
wahisani ambao ni Benki ya Dunia.
Mradi huo umepangiwa kuwanufaisha, wanakijiji katika vijiji vinne vya Bumbuli Mission, Bumbuli Kaya, Mboki na Kwamanolo na ulikuwa uanze kutoa huduma ya maji kuanzia Kijiji cha Kwamanolo.
“Ilipangwa kujenga tanki lenye uwezo wa kuhifadhi
maji lita 135,000, lakini mkandarasi aliamua kujenga tangi lenye uwezo
wa kuhifadhi lita 90,000 ili kuuunganisha na tanki la zamani lenye uwezo
huohuo lakini mkandarasi hakuunganisha matanki hayo jambo ambalo ni
kosa’’ alisema..
Alisema fedha zilizotumika na thamani halisi ya
mradi ni tofauti na kwamba ni vigumu kwake kuamini kwamba mradi huo
utatekelezwa kama ulivyokusudiwa awali.
Alisema ni afadhali asipokee kwanza mradi huo ili
taratibu zingine za kuchunguza zifanyike kama ni kweli mradi huo
utasambaza maji ya kutosha.
chanzo: Mwananchi
chanzo: Mwananchi