Monday 8 July 2013

Wafahamishe wengine yale mazuri


                 

 
Na Stephen Maina  (email the author)

Posted  Jumapili,Julai7  2013  saa 5:14 AM
Kwa ufupi
“Alisema mbali na suala la menejimenti lakini pia kulikuwa na matatizo ya mvua kubwa kunyesha kuliko kiwango kilichotarajiwa.”


Endelea kujifunza Kiswahili na kama ikiwezekana uwafahamishe wengine yale mazuri unayoyapata unaposoma makala haya. Angalia sentensi zifuatazo:
“Alisema mbali na suala la menejimenti lakini pia kulikuwa na matatizo ya mvua kubwa kunyesha kuliko kiwango kilichotarajiwa.”
Matumizi ya neno ‘lakini’ mara nyingi hutumika visivyo. ‘Lakini’ hutumika kama ni kiunganishi cha mafungu ya maneno katika sentensi. Lilivyotumika sasa ni makosa. Tunaweza kuliondoa neno ‘lakini’ bila kuathiri maana iliyokusudiwa. Kwa mfano:
“Alitaka kujua mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara za ndani ‘ring roads’(barabara za pembezoni) katika jiji hilo.”
Hakuna umuhimu wa kutumia maneno ya Kiingereza kama ‘ring roads’ kwani wasomiaji wa magazeti ya Kiswahili wana elimu ya kawaida. Hivyo mwandishi alitakiwa kutumia maneno kama ‘barabara za pembezoni’ na kwa ufafanuzi kutumia ‘ring roads’ ingesaidia kushadidia hoja hiyo.
“ Katika shoo hiyo, itasindikizwa na Ben Pol anayewania tuzo sita kwenye Kil Muzic Awards.”
Siyo kawaida kwa msanii kusindikiza shoo bali ni msanii hushiriki katika shoo. Kwa hiyo isomeke,
“Katika shoo hiyo, itahudhuriwa na au atakuwapo Ben Pol anayewania tuzo sita kwenye Kili Muzic Awards.”
“Mwigizaji anayefanya vizuri kwenye tasnia hiyo kwa sasa Recho Haule au Recho Saganda amesema yeye ni jike la shamba.”
Maana ya ‘tasnia ‘ ni shughuli za biashara zenye kutoa huduma kama vile utalii au usafirishaji. Uigizaji ni tasnia ? Hii ni sanaa yenye malengo mawili. Kwanza ni burudani na pili ni biashara. Kwa kuwa ni sanaa kwa sehemu kubwa ni burudani.
Ingefaa iandikwe,
Mwigizaji anayefanya vizuri kwenye sanaa kwa sasa ni Recho Haule au Recho Saganda amesema yeye ni jike la shamba.”
Unaweza kuendelea kuisoma kupitia

 http://www.mwananchi.co.tz/kolamu/lugha-yetu/Wafahamishe-wengine-yale-mazuri/-/1614740/1907632/-/crebyj/-/index.html