Kwa ufupi
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Katiba la
Wilaya ya Sumbawanga Prof. Baregu alionyesha dhairi kukerwa na kauli
hiyo ya kusema “wasomi wanaipeleka nchi kusikojulikana” ambayo
ilijitokeza mara kadhaa kwa watu waliokuwa wakichangia rasimu hiyo ya
katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Rukwa. MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Prof. Mwesiga Baregu amewataka wajumbe wa mabaraza ya katiba kujenga
hoja kuhusu muundo wa Serikali wanayoitaka badala ya kung’ang’ana
wakiwalaumu wasomi kwa kudai wanaipeleka nchi kusikojulikana kutokana na
wengi wao kuonyesha wanataka Serikali tatu.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Katiba la
Wilaya ya Sumbawanga Prof. Baregu alionyesha dhairi kukerwa na kauli
hiyo ya kusema “wasomi wanaipeleka nchi kusikojulikana” ambayo
ilijitokeza mara kadhaa kwa watu waliokuwa wakichangia rasimu hiyo ya
katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Hoja za kusema wasomi mnatupeleka kusikojulikana
siyo sahihi kama hamtaki serikali tatu jengeni hoja ya muundo wa
serikali mnazotaka. Hii ni katiba ya Watanzania wote siyo wasomi
pekee.......sisi tutazichukuwa hoja zenu na kwenda kuzifanyia kazi”
alisema Prof. Baregu.
Awali diwani wa Kata ya Muze, Kalolo Ntilo alisema
kuwa suala muungano wa Serikali tatu ambalo rasimu imependekeza
hakubaliani nalo ila anataka kuwepo Serikali mbili za Tanzania bara na
Zanzibar ambazo zitaunda muungano wa nchi hizo mbili huku wakiwatupia
lawama wasomi kwa kudai wanataka kuwepo Serikali tatu ambazo athari zake
ni kuvunjika kwa muungano miaka kadhaa ijayo.
Diwani huyo alisema suala la serikali tatu
linahitaji mjadala wa kipekee utakajumuisha Watanzania wote hivyo kwa
maoni yake haoni sababu ya katiba ijayo kuwa na muundo wa Serikali hizo
ambazo zinapigiwa chepuo na baadhi ya wananchi wakiwamo wasomi.
Mkazi wa Kaengesa, Lazaro Muntama alisema kuwa ili
kunusuru muungano kutovunjika ipo haja ya kuwepo kwa Serikali tatu
yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano ambapo alipinga hoja za baadhi
ya wajumbe zinazoeleza kuendesha serikali hizo ni gharama kubwa.
“imefika wakati sasa na sisi watu wa bara tunataka
Serikali yetu ya Tanganyika ili tuwe na muundo wa Serikali tatu siyo
mbili huku ni kujizudhuru haki yetu.