Kwa ufupi
Mlugu alisema baada ya kufika Dar es Salaam,
vijana hao wamejikuta wakiingia kwenye biashara hizo kutokana na
unyanyasaji na ujira mdogo.
Utafiti unaonyesha vijana wanaojihusisha na vitendo hivyo wanatolewa vijijini
Dar es Salaam. Asilimia 65 ya
vijana kata za Buguruni na Vingunguti wapo hatarini kupata maambukizi ya
virusi vya Ukimwi kutokana na kujihusisha na biashara ya ushoga na
uchangudoa.
Katika utafiti uliofanywa na Shirika la Ushauri
kwa Familia (CAFLO) mwishoni mwa mwaka jana, uneonyesha idadi kubwa ya
vijana hao ni wenye umri kuanzia miaka 12 na kuendelea.
Akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo
vijana na watu wanaoishi na VVU kutoka maeneo hayo juzi, Mwenyekiti wa
shirika hilo, Mariam Mlugu, alisema idadi kubwa ya vijana hao ni wale
waliochukuliwa kutoka mikoani kufanya kazi za ndani.
Mlugu alisema baada ya kufika Dar es Salaam,
vijana hao wamejikuta wakiingia kwenye biashara hizo kutokana na
unyanyasaji na ujira mdogo.
Alisema baada ya utafiti huo waliwasiliana na
Kamati ya Ukimwi Manispaa ya Ilala ambayo ilikubali kuliwezesha shirika
hilo kutoa mafunzo kwa vijana na wanaoishi na VVU, ili wabuni na
kutafuta fursa mbalimbali kujiletea maendeleo.
Pia, Mlugu alisema baadhi ya familia na jamii
zimekuwa zikikosa fursa kufanya shughuli halali na kuamua kujiingiza
kwenye kazi hatarishi, kama biashara ya ngono na mapenzi ya jinsia moja
kwa lengo la kujipatia kipato.
Awali, Mkurugenzi wa utawala wa shirika hilo,
Dennis Mikongoti, alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo
watu wanaoishi na VVU na Ukimwi na ambao wapo hatarini kupata magonjwa
hayo, ili wapambane na umaskini wa kipato ambao ndiyo unachangia kwa
kasi maambukizi hayo. Naye
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Ilala,
Malcela Msawanga, aliwaasa washiriki hao kutumia mafunzo hayo
kuwaelimisha wenzao ambao hawakupata fursa hiyo.