Na Bakari Kiango
(email the author)
Posted Jumatatu,Julai22 2013 saa 21:23 PM
Kwa ufupi
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar
es Salaam, limepeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali maji yanayodhaniwa
kuwa ni tindikali aliyomwagiwa mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohammed Saad kwa ajili ya uchunguzi.
Mmoja wa Ofisa wa Polisi, ambaye hakutaka kutaja
jina lake aliliambia gazeti hili jana kuwa baada ya tukio hilo polisi
wameamua kuyachukua maji hayo na kuyapeleka huko kwa uchunguzi ili
kubaini ndani yake yalikuwa na nini.
Tukio hilo la kumwagiwa maji hayo lilitokea Julai
20 mwaka huu saa 1 usiku karibu na Kituo cha Polisi cha Osterbay
wilayani Kinondoni, wakati Saad akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wake katika duka lake jipya lililopo katika maeneo hayo.
“Majibu yatakayotoka kwa Mkemia Mkuu yatatusaidia katika upelelezi wetu katika jambo hili,” alisema Ofisa huyo na kuongeza kuwa.
“Hadi sasa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa
kutokana na tukio hili huku polisi wakiendelea na msako mkali wa
kuwabaini wahusika.”
Alidokeza kuwa kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa
Saad wanasema mgonjwa wao anaendelea vizuri na matibabu katika moja ya
hospitali aliyolazwa, huku polisi wakimsubiri apate ahueni kwa ajili ya
kumfanyia mahojiano juu ya tukio hilo.
Katika hatua nyingine, polisi kanda hiyo leo
wanatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi
kuhusu suala kulipuka kwa bomu katika mkutano wa Chadema.
Tukio hilo lilitokea Julai 22 mwaka huu maeneo ya
Viwanja vya Sahara Mabibo wakati kitu kinachodhaniwa ni bomu kilichokuwa
ndani ya gari la polisi kilirushwa katika mkutano huo.
Chanzo: Mwananchi news paper
Chanzo: Mwananchi news paper