Tuesday 18 June 2013

USALAMA WETU UKO SHAKANI


 
Majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea jijini Arusha. 


Posted  Jumatatu,Juni17  2013  saa 21:51 PM
Kwa ufupi

Kwanza tunawapa pole wale wote ambao wameguswa kwa namna moja au nyingine na tukio hili; wale walioondokewa na wapendwa wao, waliojeruhiwa na uongozi wa Chadema.


Nchi yetu imeandika tena historia mbaya katika masuala ya usalama kutokanana mlipuko wa bomu uliotokea jijini Arusha Jumamosi iliyopita, wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilipokuwa kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Viwanja vya Soweto jijini humo.
Taarifa zinasema watu kadhaa wamepoteza maisha hadi sasa japokuwa idadi yao bado haijafahamika kutokana na mamlaka mbalimbali kutoa taarifa zinazokinzana huku watu kwa makumi nao wakijeruhiwa, miongoni mwao vibaya.
Bomu hilo lililipuka muda wa jioni yapata saa 12 muda mfupi kabla ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo na kusababisha taharuki kubwa na baadaye sintofahamu miongoni mwa wakazi wa Arusha na Tanzania nzima kwa ujumla.
Itakumbukwa kwamba hili ni tukio la pili katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu kutokea jijini Arusha katika mkusanyiko wa watu, kwani Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit jijini Arusha na kuua watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kwanza tunawapa pole wale wote ambao wameguswa kwa namna moja au nyingine na tukio hili; wale walioondokewa na wapendwa wao, waliojeruhiwa na uongozi wa Chadema.
Ni tukio baya, linalosikitisha ambalo linapaswa kulaaniwa na kila mpenda amani wa nchi yetu. Kwa mara nyingine amani ya nchi yetu imetiwa doa.
Tafsiri ya tukio hili ni kwamba usalama wetu sasa kama Watanzania uko shakani. Ilitarajiwa kwamba baada ya tukio la mwanzoni mwa mwezi jana, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vingefanya kazi kubwa ya kuchunguza na kubaini chimbuko la uhalifu huu wenye sura ya ugaidi na kuudhibiti kabla haujaathiri watu wengi zaidi!. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba umetoekea mlipuko mwingine katika muda mfupi tangu utokee wa kwanza katika mji huo huo na katika mazingira yanayofanana na yale ya awali kwa maana ya mkusanyiko mkubwa wa watu.
Hapa kuna maswali mengi yanayohitaji majawabu sahihi kwamba vyombo vyetu vya usalama vimelifanyia kazi kwa kiasi gani tukio la Mei 5 mwaka huu, kwa lengo la kupata taarifa za kuwezesha kuchukua hatua za kiusalama kwa wakazi wa Arusha?
Kutokea tena kwa mlipuko Jumamosi jioni, ni dhahiri kwamba Wanausalama wetu wameshindwa kuwalinda wakazi wa Arusha na huu ni udhaifu mkubwa katika mifumo ya usalama wa nchi yetu na watu wake.
Tunasema hivi tukirejea matukio kadhaa ya uhalifu ambayo Jeshi la Polisi liliyaundia tume kwa ajili ya kuyachunguza ili kuwezesha hatua kuchukuliwa. Lakini ni dhahiri kwamba tume hizi ama zimeshindwa kufanya kazi yake na kutoa taarifa zenye tija au kama taarifa zake zipo basi hazifanyiwi kazi.
Tume hizi ni kama hazina tija na badala yake zinaongeza mzigo wa gharama kwa walipakodi.
Katika mazingira haya ni dhahiri tunahitaji mabadiliko makubwa (reforms) katika utendaji wa polisi na vyombo vingine vya usalama. Vyombo hivi vinapaswa kufahamu kwamba vina dhamana ya kuhakikisha wananchi wanakuwa salama. Hiyo ndiyo kazi yake na jukumu lake kubwa na siyo kin