Kama ni mfuatiliaji mzuri wa kipindi cha Skonga, utamkumbuka Happiness
Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya
kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu
kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.
Happy
(19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya
Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule
iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte
International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na
mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi
Happy. Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa
na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo.
Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo
Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.
Kipindi
ambacho Happy yupo kwenye likizo ndefu, alipata wakati mgumu wa
kutokuwa na kitu cha kufanya, hivyo Happy aliamua kujihusisha na masuala
ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la Miss Dodoma, na Miss Kanda ya
Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya Miss Tanzania.
Akiwa
Miss Tanzania, Happy alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuingia Nusu Fainali
ya mashindano hayo kwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013.
Ndani
ya kambi ya Miss Tanzania, Happiness Watimanywa amekuwa mwiba kwa
warembo wengine 29 wanaowania taji hilo kwani amekuwa akionesha uwezo wa
hali ya juu kuanzia kwenye kipaji hata michezo, ukiachilia mbali upeo
mkubwa alio nao
SOURCE: FULL SHANGWE
HABARI ZAIDI TEMBELEA: http://othmanmichuzi.blogspot.no/2013/09/happiness-watimanywa-ndie-redds-miss.html