Friday 6 September 2013

Jen.Davis Mwamunyange:Vikosi vya JWTZ vinapaswa kuendeleza mafunzo na mazoezi kujiweka imara.


                      
 Mkuu wa majeshi  jenerali Davis Mwamunyange amesema vikosi vya jeshi la wananchi nchini vinapaswa kuendeleza utaratibu wa mazoezi  na mafunzo ya mara kwa mara ili  kujiweka imara kwa ulinzi wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza  wakati  wa uzinduzi  wa mazoezi ya vikosi vya nchi kavu katika  brigedi ya mbuni  yaliyopewa jina la operesheni ''kuwa imara
'' jenerali mwamunyange amesema jeshi la tanzania limejenga heshima ya kimataifa hivyo ni lazima kuitunza heshima hiyo.
Naye meja Jenerali Salum Kijuu ambaye ndiye mkuu wa vikosi vya nchi kavu anasema lengo la mazoezi hayo ni kuwandaa maafisa na askari kimafunzo ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na adui katika mapigano ya nchi kavu.
 Kuhusu uhusiano wa kijeshi baina ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo nchi ya Rwanda,mkuu wa operesheni na
Mafunzo kamandi ya jeshi la nchi kavu brigedia jenerali Zoma Kongo anasema uhusiano ni mzuri  na nchi hizo zimeendelea kushirikiana  katika mafunzo  mbalimbali ya  kijeshi.

source: ITV -Daima