Wednesday, 11 September 2013

Korodani ya wanaume na majukumu ya mzazi

 
Imebadilishwa: 11 Septemba, 2013 - Saa 11:19 GMT
 
Wanasayansi wanasema kuwa kuna uhusiano kati ya ukubwa au udogo wa Korodani (Testicles) za baba na uwezo wa baba kutekeleza majukumu yake kama mzazi wa watoto wao.
Watafiti katika chuo kikuu cha Emory nchini Marekani, wanasema kuwa wanaume walio na Korodani ndogo huenda wakayachukualia majukumu yao kwa uzito na hata kujihusisha na kumbadilisha mtoto nepi, kumlisha na hata kumuogesha mtoto.
Pia uligundua kuwa utofauti katika picha ya ubongo wa baba wakitizama picha za waoto wao, ilihusishwa na ukubwa au udogo wa Korodani.
Lakini mambo mengine ya kitamaduni yanaweza kuchangia kwenye uhusiano kati ya Korodani na majukumu ya baba kwa mwanawe.
Uasherati na ukubwa wa korodani zinajulikamna kuwa na uhusiano mkubwa kwa wanyama , wale walio Korodani kubwa hujamiiana na wanyama wengi kinyume na walio na Korodonani ndogo.
Watafiti walikuwa wanachunguza nadharia kuhusu ikiwa wanaume hutumia muda zaidi katika kuwa na mahusiano ya kimapenzi au kulea watoto wao. Wazo lao likiwa kwamba wanaume walio na Korodani kubwa hutumia muda wao katika kuzaa watoto wengi kuliko katika kuwalea watoto hao.
Utafiti huo ulichunguza uhusiano kati ya ukubwa wa Korodani na mfumo wa uzazi katika wananume 70 waliokuwa na watoto walio kati ya umri wa mwaka mmoja na miwili.
Watafiti waliwapiga wanaume hao picha ya ubongo wakiwa wanatizama picha za wanao.
Utafiti wao ulionyesha kuwa wanaume wenye Korodani ndogo walionekana kuwa makini katika malezi kuliko wale wenye kubwa.
Wale waliokuwa na Korodani ndogo walionekana kuwa na wazazi wazuri wanaojihusisha na kubadilisha mtoto nepi na kumuogesha, yaani alijihusisha vyema katika majukumu ya mzazi.
Mmoja wa watafiti alisema kuwa uchunguzi wao unaonyesha kwamba kuna baadhi ya wanaume ambao ni wazazi wazuri tu na ambao wanajihusisha na majukumu ya ulezi kuliko wengine.
Watafiti hao waliona kuwa ukubwa au udogo wa Korodani unaweza kuathiri tabia za mtu, lakini haijulikani kama hatua ya kumpata mtoto hubadili mawazo na mienendo ya baba.

source: BBC swahili