Serikali imefunga mashine mpya na za kisasa zenye uwezo wa kubaini aina
yoyote ya dawa za kulevya na nyara za serikali kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-salaam, lengo likiwa ni
kudhibiti uingizwaji na upitishwaji wa mizigo uwanjani hapo,ambapo
kuanzia sasa mizigo yote inayoingia na kutoka itakaguliwa.
Waziri wa uchukuzi Mheshimiwa Dk Harison Mwakyembe
ameyasema hayo jijini Dar-es-Salaam,mara baada ya kutembelea uwanja huo
kwa mara ya pili ili kuona zoezi la ufungwaji wa mashine za kisasa zenye
uwezo kutambua dawa za kulevya na nyala nyingine za serikali.
Meneja wa usala wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere Bwana Clence Jingu,amesema kuwa kufungwa kwa mashine hiyo
ambayo itakuwa ikijiongoza yenyewe kwa kukagua mizigo ya abiria
wanaoingia na wanaosafiri tofauti za zamani ambapo mizigo iliyokuwa
ikiingia ilikuwa haikaguliwi.
Awali akiwa uwanjani hapo waziri Mwakyembe
amewaagiza wasimamizi wa uwanja huo,kuhakikisha kuwa ombaomba wote
wanaozagaa uwanjani hapo wanaondolewa mara moja,kwani uwanja huo ndiyo
kioo na sura ya Tanzania ambapo ITV ilishuhudia baadhi ya abiria
wakipita na kuwapatia ombaomba hao kitu chochote.
Katika tukio lingine waziri Mwakyembe alizuru
ghafla kwenye mizani iliyopo maili moja kibaha mkoani Pwani, mara baada
ya kupigiwa simu na mawaziri wa ulinzi na wa uchukuzi wa Zambia,wakidai
kuwa raia wao wamezuiliwa kuondoka kwa mabasi yao manne yaliyopitia
bandari ya Dar-es-Salaam kwa madai kuwa yamezidi viwango vya urefu kwa
barabara za Tanzania ambapo walitakiwa kulipa faini ya dola za marekani
ishirini elfu kwa kila basi moja.
Source: ITV news