Kwa ufupi
Makamba aliyasema hayo jana mjini hapa wakati
akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wadau mbalimbali wa taasisi za fedha
ikiwepo Benki Kuu ya Tanzania(BOT).
Morogoro.Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba amesema katika kipindi hiki cha sayansi na
teknolojia,mitandao imekuwa ikihusika hivyo ni lazima iwe salama kwa
kudhibiti wizi unaoendelea kufanyika nchini.
Makamba aliyasema hayo jana mjini hapa wakati
akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wadau mbalimbali wa taasisi za fedha
ikiwepo Benki Kuu ya Tanzania(BOT), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),
Mifuko ya hifadhi ya jamii, Ofisi ya mkaguzi, maafisa kutoka taasisi na
ofisi za Serikali pamoja na wadau wa mitandao ya simu .
Mafunzo hayo yalifadhiliwa na Shirika la ISACA
Tanzania Chapter linaloshughulikia wizi wa mitandaoni kwa nchi za Afrika
Mashariki lenye makao makuu Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya
Norway Registerd Development (NRD) ambayo inashughulika na usalama wa
mitandao.
source : Mwananchi
source : Mwananchi