Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi
wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya
kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano ya
Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani
.Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa
maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na
baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya
kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa
katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya
utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani
Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
Watalaamu
wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini wakimueleza
Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba hayo
Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na
baadhi ya vibarua wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya
kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji,
Pwani.
Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
Mmiliki wa blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda naye akiwa katika ziara hiyo eneo la Nyamwage, Rufiji.
Kambi ya wafanyakazi wa kamapouni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
Waandishi
wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo
zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama,
zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani
Mkuranga, Pwani
Baadhi
ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya
kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa
baharini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO
BLOG.