Kwa ufupi
- Aliongeza kuwa magari yanayoruhusiwa kupita bure katika vivuko hivyo ni ya Serikali na wagonjwa.
Mchezo mchafu unaelezwa kuikosesha Serikali mamilioni ya fedha kwenye vivuko vya Magogoni na Kigamboni, Dar es Salaam.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni, umegundua ukwepaji malipo unaofanywa na wenye magari.
Pia, kuna wizi wa tiketi unadaiwa kufanywa na wakata tiketi.
Hata hivyo, Kitengo cha Wakala wa Ufundi na Umeme
(Temesa), kinaonekana kutokuwa na habari ya wizi huo, huku kikificha
taarifa za mapato ya vivuko hivyo.
Ofisa Habari wa Temesa, Theresia Mwami, alisema kanuni haziruhusu kuweka wazi mapato hayo na kwamba, kanuni zote zinafuatiliwa.
“Serikali inaendeshwa na kanuni na taratibu… kama
Serikali inataka kujua hizo taarifa itazipata kwenye taasisi yake. Kama
ni nauli zimebadikwa kwenye ubao wa matangazo na kila mwananchi anapaswa
kulipa nauli kwa kiwango hicho, siyo nje ya hapo,” alisema Mwami.
Aliongeza kuwa magari yanayoruhusiwa kupita bure katika vivuko hivyo ni ya Serikali na wagonjwa.
“Kwa sasa tuna utaratibu wa tiketi za ku- scan, kwa hiyo kila gari linapopita linaangaliwa kama limelipa,” alisema.
Kwa mujibu wa Temesa, nauli za kivuko kwa watu wazima ni Sh200 na watoto hadi miaka 14 ni Sh50, huku wanafunzi wakipanda bure.
Kwa upande wa vyombo vya usafiri, baiskeli ni
Sh300, pikipiki Sh500, mzigo chini ya kilo 50 Sh200, zaidi ya hapo ni
Sh500. Mikokoteni inatozwa Sh1,500, pikipiki za magurudumu matatu
Sh1,800, Bajaj Sh1,300.
Kwa magari aina ya saluni Sh1,500, madogo Sh2,000,
mabasi madogo Sh3,500, magari ya tani 2.0 hadi 3.5 na trekta lisilo na
tela Sh7,500. Kwa upande wa wanyama, ng’ombe anavushwa kwa Sh2,000,
wanyama wengine wa kufugwa Sh1,000.
Jinsi mchezo unavyofanyika uchunguzi uliofanyika
kwa wiki kadhaa umebaini kuhusika kwa polisi na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), ambao huruhusu baadhi ya magari kutofuata utaratibu.
“Utakuta tunalipia magari yetu na kupanga foleni ya kuingia
kwenye vivuko, lakini wengine wanapitishwa bure kwenye geti la jeshi,”
anasema Ramadhan Juma anayeishi Kigamboni.
Mwandishi wa habari hizi alipofika eneo la
kivukoni Kigamboni kwenye geti hilo, alikuta foleni ya magari ya jeshi,
Serikali na magari binafsi.
Kwa upande mwingine kuna foleni kubwa ya magari binafsi yanayolipia, ambayo pia hukaguliwa.
“Ni vigumu kusema magari mangapi yanayopita bure
hapa, lakini tangu asubuhi hadi jioni yanapita mamia ya magari. Sasa
kama kila gari linatakiwa kulipa Sh1,500 ni kiasi gani kinapotea kwa
siku?” Alihoji Sadiki Madembwe, anayefanya biashara eneo hilo.
Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa JWTZ, Meja Eric Komba, amekanusha madai ya geti la wanajeshi kutumika kupitisha bure magari binafsi.
“Unajua kuna wanajeshi wanaaoishi Kigamboni na
kule pia tuna kambi yetu, kwa hiyo magari ya jeshi yanapita na magari
binafsi ya wanajeshi pia yanapita bure. Sasa watu wakiona vile wanadhani
kuna magari ya raia yanayopitishwa, siyo kweli,” alikanusha Meja Komba
na kuongeza:
“Mimi nimefanya uchunguzi, hicho kitu hakipo na
kama kuna mwanajeshi anafanya hivyo mlete ushahidi tu, tutamfukuza kazi.
Isitoshe, sisi tuna ushirikiano mzuri na wananchi kwa hiyo hatuna
tatizo pale.”
Mmoja wa waliowahi kufanya kazi ya kukatisha
tiketi katika vivuko hivyo mwaka mmoja uliopita ambaye hakutaka kutajwa,
alisema kuna wizi mkubwa katika uuzaji wa tiketi.
“Kwa sasa hivi ni tofauti kwa sababu tiketi
zimetengenezwa kwa mfumo wa kompyuta na abiria akishanunua, inakaguliwa
kwa ‘Scanner’. Lakini zamani wakaguzi walizikusanya zile tiketi na
kuziuza upya,” alisema na kuongeza:
“Hata sasa, licha ya Scanner bado tiketi
zinakusanywa na kurudishwa tena dirishani kuuzwa. Kwa sababu abiria
akishanunua tiketi humkabidhi mkaguzi ambaye huikagua na kuitupa kwenye
ndoo ya taka. Hapo abiria hafuatilii tena kama Scanner imelia au
haijalia kwa sababu tiketi hairudishwi.”
Hadi sasa kuna vivuko viwili yaani Mv Magogoni
kinachokadiriwa kubeba abiria 2,000 kwa wakati mmoja na magari madogo
20, pikipiki, baiskeli na mikokoteni.
Huku Kivuko cha Mv Kigamboni kinakadiriwa kubeba abiria 800 hadi 1,000 kwa wakati mmoja, magari, mikokoteni na baiskeli.
liongeza kuwa baadhi ya watu hupita bure na magari na jamaa zao kwa kujuana na walinzi.
liongeza kuwa baadhi ya watu hupita bure na magari na jamaa zao kwa kujuana na walinzi.
“Michezo huwa unafanyika zaidi muda wa jioni, utakuta mtu pale anaondoka hadi na Sh100,000 kwa siku,” alisema.
Akizungumzia hali hiyo, Mbunge wa Kigamboni, Dk
Faustine Ndugulile, alisema ameshawaeleza Temesa lakini haoni hatua
madhubuti zikichukuliwa.
“Nikiwa mbunge nimesikia malalamiko mengi pale
kwenye vivuko, nimechukua hatua ya kukutana na maofisa wa Temesa
kuwaeleza kero hizo,” alisema Dk Ndungulile na kuongeza:
“Pale kuna magari kama 10 ya kudumu yanayotakiwa
kupita bure yaani ya wanajeshi, Serikali na magari ya wagonjwa. Lakini
magari mengi mno yanapita bure.”
Akitaja baadhi ya hoja zake kwa Temesa, Dk
Ndugulile alisema licha ya kuboreshwa kwa tiketi za sasa, aliwataka
waanzishe tiketi za msimu kwa wavukaji wa kudumu jambo ambalo
halijatekelezwa hadi sasa.
“Ni kweli sasa wameboresha utoaji tiketi, lakini
niliwataka waainishe tiketi za msimu. Kuna watu wanaovuka kila siku
wanaweza kulipa kwa mwezi. Vilevile waboreshe mfumo wa kuingilia na
kutoka,” alisema Dk Ndugulile.
source: Mwananchi
source: Mwananchi