Posted Alhamisi,Agosti29 2013 saa 12:50 PM
Kwa ufupi
Watafiti wa masuala ya kiuchumi wanasema
bandari hii ni lango kuu la biashara ya kimataifa kwa nchi za Afrika
Mashariki na Kati ambazo hazina bahari na kama ingekuwa na ufanisi kama
ilivyo Bandari ya Mombasa, uchumi wa Tanzania ungeingiza takriban Dola
za Marekani 1.8 bilioni kwa mwaka (Sh2.88 trilioni) sawa na asilimia 7
ya Pato la Taifa (GDP) kwa sasa.
Bandari ya Dar es Salaam; rasilimali nyingine ambayo Tanzania imejaliwa katika mwambao wa Bahari ya Hindi.
Watafiti wa masuala ya kiuchumi wanasema bandari
hii ni lango kuu la biashara ya kimataifa kwa nchi za Afrika Mashariki
na Kati ambazo hazina bahari na kama ingekuwa na ufanisi kama ilivyo
Bandari ya Mombasa, uchumi wa Tanzania ungeingiza takriban Dola za
Marekani 1.8 bilioni kwa mwaka (Sh2.88 trilioni) sawa na asilimia 7 ya
Pato la Taifa (GDP) kwa sasa.
Mbali na hayo linapokuja suala la usafirishaji wa
shehena za mizigo kwenda au kutoka ughabuni; Zambia, Uganda, Rwanda,
Burundi, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) na Malawi wanatumia
Bandari ya Dar es Salaam ili kufikia lengo hilo.
Zambia inatumia bandari hiyo kwa asilimia 46.6, Burundi (9.1), Rwanda (8.5), Malawi(4.1) na nyingine asilimia 9.8.
Takribani asilimia 90 ya biashara ya kimataifa ya Tanzania hupita katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wakati bandari hiyo ikionekana kuwa muhimu kiasi
hicho, hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti kuwa nchi za Uganda na
Rwanda zitasitisha kutoitumia bandari hiyo kuanzia mwezi Septemba.
Kwa mujibu wa Chama cha Wasafirashaji wa Mafuta
nchini(Tatoa), nchi hizo zimekuwa zikiilalamikia bandari hiyo lakini
hakuna hatua zozote zimechukuliwa na serikali kutatua matatizo hayo.
Takriban asilimia 90 ya biashara ya kimataifa ya Tanzania hupita katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wakati bandari hiyo ikionekana kuwa muhimu kiasi
hicho, hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti kuwa nchi za Uganda na
Rwanda zitasitisha kutoitumia bandari hiyo kuanzia mwezi Septemba.
Kwa mujibu wa Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta
nchini(Tatoa), nchi hizo zimekuwa zikiilalamikia bandari hiyo lakini
hakuna hatua zozote zimechukuliwa na Serikali kutatua matatizo hayo.
Moja ya malalamiko yanayotajwa ni wafanyabiashara
kucheleweshewa mizigo yao katika bandari hiyo na kuwapo kwa vizuizi
vingi kwenye barabara za Tanzania.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe anasema
nchi hizo haziwezi kujitoa katika Bandari ya Dar es Salaam kwani umbali
kutoka Kigali hadi Dar es Salaam ni zaidi ya kilometa 1,460) wakati
kutoka Kigali hadi Mombasa ni kilometa 1,704 ilipo bandari nyingine
ambayo inatarajiwa kutumiwa na Rwanda.
Waziri anabainisha kwamba inachukua saa 18 kutoka Dar es Salaam hadi Kigali wakati Kigali mpaka Mombasa ni saa 25.
Dk Mwakyembe anakiri kwamba kuna vizuizi 56 katika barabara inayotoka Dar es Salaam hadi Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania.
Kutokana na vizuizi hivyo Serikali ina mpango wa
kuvipunguza na kubaki vitatu, lakini pia anasema atawasiliana na waziri
mwenzake wa Rwanda mwenye dhamana ya Uchukuzi kwa ajili ya kuzungumzia
suala hilo.
Rwanda, Uganda kujenga reli
Wakati bandari hiyo ikisifika kwa kutokuwa na
tija, Juni Rais Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na
Uhuru Kenyatta wa Kenya walikutana mjini Entebe Uganda na kwa pamoja
walipitisha uamuzi wa kujenga reli itakayounganisha Miji ya Mombasa,
Kampala na Kigali.
Ujenzi wa reli hiyo una thamani ya Dola 13 bilioni
za Marekani na unatarajiwa kukamilika mwaka 2018 na mpango huo unatajwa
kuwa muhimu katika kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mombasa hadi
Kigali.
Ujenzi huo bila shaka utaleta changamoto katika
Bandari ya Dar es Salaam ambayo inaonekana kuwa na matatizo chungu
nzima, ambayo yamesababisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
kukataa kupitisha ripoti ya Hesabu ya Mamlaka ya Bandari (PTA) kutokana
na ubadhilifu wa Sh57.6 bilioni.
Kwa upande wa Tanzania, Dk Mwakyembe anasema
mikakati inaendelea ya kuiboresha reli ya kati na itakapokamilika
itasaidia kusafirisha mizigo kupeleka maeneo mbalimbali zikiwamo nchi
jirani.
Waziri Mwakyembe anafafanua kuwa watahakikisha
hadi kufika mwaka 2015 Bandari ya Dar es Salaam, inakuwa na uwezo wa
kuingiza tani milioni 12 hadi tani milioni 18 kwa mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti kuhusu
Kuondoa Umaskini (Repoa), Profesa Samuel Wangwe anasema ujenzi wa reli
ya nchi hizo tatu hautaathiri sana uchumi kwani kuna umbali mrefu kutoka
Mombasa hadi Kigali.
Profesa Wangwe anasema kuna umuhimu wa kujenga
reli inayotoka Kigoma kwenda nchi za Kongo (DRC) na Burundi ili
kurahisisha usafirishaji wa mizigo.
Profesa huyo anasema Bandari ya Dar es Salaam
inaweza kuwa kitovu cha biashara katika nchi za ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati, lakini ili ifikia katika kiwango hicho hakuna budi
kufanya kazi kisasa.
“Mizigo ishughulikiwe haraka na watumie taknolojia za kisasa,” anasema Profesa Wangwe.
Vizuizi barabarani
Profesa Wangwe anasema ili kuongeza ufanisi zaidi,
mambo matatu yanapaswa kutazamwa ambayo ni kuondoa rushwa, kutumia
teknolojia ya kisasa katika bandari hiyo na kupunguza vizuizi vya
ukaguzi barabarani.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa
Joseph Mbele anasema Tanzania inapaswa kufanya utafiti ili kupunguza
gharama za uendeshaji na kuleta ushindani.
Utafiti uliofanywa na mtandao unaojihusisha na
ukaguzi wa hesabu KMPG na Benki ya Dunia(WB) unaonyesha kwamba Mei na
Juni 2012, meli zilizokuwa zimebeba makontena zilikuwa zinapanga foleni
kwa wastani wa siku 10 ili kusubiri gati katika Bandari ya Dar es
Salaam, wakati muda wa kusubiri ulikuwa chini ya siku moja katika
Bandari ya Mombasa.
Pia utafiti huo unasema siyo tu kwamba Bandari ya
Dar es Salaam haina ufanisi, lakini pia ina gharama kubwa kwa asilimia
74 kuliko Mombasa na kusababisha kampuni nyingi za meli, kulazimika
kulipa ada zaidi kwa mawakala kuliko Bandari ya Mombasa.
Ripoti hiyo inaweka wazi kuwa kama hali ya sasa
haitapatiwa ufumbuzi, Bandari ya Dar es Salaam inaweza kupoteza nafasi
yake katika biashara ya ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
source : Mwananchi
source : Mwananchi