Moto mkubwa umeteketeza jengo la baa ya Samaki Samaki
Mbezi Beach
Jijini Dar Es Salaam na kuleta taharuki kwa wamiliki wa
majengo jirani jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda,moto huo ulioanza majira ya
saa tano umelipuka gafla na kusambaa mara baada ya tingatinga lililokuwa
likibomoa kupisha njia ya ujenzi wa bomba kuu la maji toka Ruvu chini
hadi jijini Dar es salaam kubomoa sehemu ya mbele ya jengo hilo huku
wakilalamikia uchelewaji wa vikosi vya zimamoto na uokoaji
Hata hivyo meneja wa jengo hilo aliyedai kuwepo hapo
wakati wa ubomoaji huo amesema chanzo ni ubishi wa opareta wa tingatinga
aliyeombwa kubomoa kwa umakini kabla ya tukio kutokana na uhalisia wa
jengo kujengwa kwa makuti, nyasi, mbao na miti mikavu huku likiwa na
mtandao wa nyaya nyingi za umeme.
Itv imeshuhudia tingatinga hilo likiendelea kubomoa
maeneo ya Mbezi beach huku baadhi ya wamiliki wa majengo yanayobomolewa
kupisha ujenzi wa bomba hilo wakiiomba serikali kuangalia kwa jicho la
upendeleo baadhi ya wamilki wa majengo ambao wanatambulika kisheria
wakiutaja kuwa ni uzembe unaotokana na watendaji wa serikali wasiokuwa
waaminifu kwa kutoa hati na vibari vya ujenzi.
source: ITV