Kwa ufupi
Alisema kikao cha baraza la mawaziri
kinatarajia kupokea ripoti kuhusu maombi hayo, ambapo tayari timu ya
maofisa wa jumuiya hiyo ilikwenda Sudan Kusini kutazama kama ina sifa za
kujiunga na jumuiya hiyo.
Arusha. Nchi za Sudani Kusini na Somalia,
zimeomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC) na tayari
mchakato wa kupitia maombi hayo umeanza.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Richard Sezibera
alitoa taarifa hiyo jana katika kikao na waandishi wa habari, wakati
akielezea kuanza kikao cha baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo.
Alisema kikao cha baraza la mawaziri kinatarajia
kupokea ripoti kuhusu maombi hayo, ambapo tayari timu ya maofisa wa
jumuiya hiyo ilikwenda Sudan Kusini kutazama kama ina sifa za kujiunga
na jumuiya hiyo.
Alisema kwa upande wa Somalia, baraza hilo
linatarajia kuridhia uamuzi wa Sekretarieti ya jumuiya ya kutuma maofisa
wake kwenda Somalia kutazama kama ipo tayari kujiunga .
Aidha alisema hadi nchi hizo kukubaliwa kuwa mwanachama kuna mchakato mrefu zitapitia.
source: Mwanachi
source: Mwanachi