31 Agosti, 2013 - Saa 13:30 GMT

Wasomi, wasanii na
wafanya-biashara wa Somalia wamekuwa wakizungumza katika mji mkuu,
Mogadishu, kwenye ile mikutano inayofanywa sehemu mbali-mbali za dunia
iitwayo TED-EX.
Mazungumzo hayo yaliyofanywa kwenye ukumbi wa
mikutano chini ya ulinzi mkubwa, yalihusu mapendekezo na ubunifu wa
kuijenga tena Somalia.Hotuba katika vikao vya TED-EX zimetolewa katika nchi zaidi ya 150.
source: BBC Swahili