Singida. Halmashauri ya Wilaya ya Singida,
imekusanya mapato ya zaidi ya Sh 22.9 bilioni kutoka katika vyanzo vyake
mbalimbali ndani ya kipindi kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Illuminata Mwenda katika taarifa yake kuhusu mapato na matumizi.
Taarifa hiyo iliwasilishwa katika kikao cha baraza
la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi cha Singida.
Alisema makusanyo hayoni sawa na asilimia 78 ya lengo la kukusanya Sh29,583,444,380 katika mwaka huo wa fedha.
Mwenda alisema katika vyanzo vya ndani, halmashauri ilikusanya zaidi ya Sh419,000,000.
“Serikali kuu imetupatia zaidi ya Sh 515.4 milioni zikiwa ni ruzuku kwa vyanzo vya mapato vilivyofutwa,” alisema.
Katika hatua nyingine, kikao hicho kimeagiza
mkaguzi wa mahesabu wa ndani, afanye ukaguzi wa vitabu vya kukusanyia
mapato kwa watendaji wote wa kata.
Pia amkague kwa makini afisa mapato wa halmashauri hiyo, anayehusika na utoaji wa vitabu vya kukusanyia mapato.
source : Mwananchi
source : Mwananchi