Jitihada
 za Mhe. Meya wa Ilala, Jerry Slaa, zinaonekana jinsi anavyojitahidi 
kupendezesha Jiji na hasa katika Manispaa yake ya Ilala kwa kuweka 
Vivutio kadhaa katika baadhi ya makutano ya barabara au mizunguko ya 
Barabara, jambo ambalo ni zuri na utambulisho pekee kwa dereve yeyote 
kutambua kuwa sasa ameingia katika anga za Manispaa ya Ilala. 
Lakini
 katika eneo hili la mzunguko huu wa makutano ya Barabara ya Jamhuri, 
eneo hili limeharibika sana kutokana na kutawaliwa na mashimo ambayo kwa
 uhakika yanapoteza maana yote ya mapambo haya yaliyowekwa eneo hili. Au
 tutafsiri kuwa yameacha kwa makusudi ili kila atakayepita eneo hili 
aweze kupunguza mwendo kwa staili ya kuogopa mashimo kumbe ndo 
anashangaa mapambo haya??????
Magari
 yote yakifika eneo hili ni lazima yapunguze mwendo ili kukwepa mashimo 
haya, jambo ambalo linasababisha msongamano mkubwa wa magari katika eneo
 hili. Mhe. Jerry Slaa, tunajua unamajukumu mengi mbele yako ya kila 
siku lakini hebu jitolee kwa hili pia basi kwa kufukia mashimo haya ili 
uweze kufikisha ujumbe kamili kwa kila anayepita eneo hili. Yangu ni 
hayo tu.
