Kwa ufupi
Akitoa maoni yake katika mchakato huo, Percival
Lwoga alisema Katiba Mpya itamke bayana kuwa suala la ardhi ni mali ya
mzawa na hata inapogundulika ni maliasili katiba ionyeshe namna
atakavyonufaika nayo.
Iringa.Wajumbe wanaoshiriki mkutano wa kukusanya
maoni ya Rasimu ya Katiba uliondaliwa na Mwavuli wa Asasi za Kiraia
Mkoani Iringa (ICSO) wamependekeza rasilimali za Taifa zitumike
kunufaisha wakazi wa maeneo husika. Akitoa maoni yake katika mchakato
huo, Percival Lwoga alisema Katiba Mpya itamke bayana kuwa suala la
ardhi ni mali ya mzawa na hata inapogundulika ni maliasili katiba
ionyeshe namna atakavyonufaika nayo. Hatua hiyo itaondoa migogoro ya
mara kwa mara inayowakumba Watanzania pindi inapobainika katika maeneo
wanayoishi kuna maliasili ikiwemo madini.