Kitu hicho ambacho kilifungwa katika boksi ambalo
liliwekwa juu a transfoma na kisha kufungwa na kamba umbali wa takribani
meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo kilisababisha taharuki kanisa hapo na
shughuli mbalimbali za ibada zilizokuwa zikiendelea kusitishwa ghafla.
Mchungaji kiongozi wa usharika huo wa kijitonyama
Ernest Kadiva amesema walipigwa na mshangao baada ya kuona uwepo wa kitu
hicho hali iliyowafanya kuwapigia simu viongozi wa polisi ili waende
kubaini kama ni bomu au la.
Naye mkuu wa upelelezi katika kanda maalum ya Dar
es Salaam Hemed Msangi ambaye alifika eneo hilo dakika chache baada ya
kugundulika kuwepo kwa kitu hicho amesema uchunguzi wa awali umebaini
kitu hicho siyo .
Hata hivyo maelezo hayo ya mkuu huyo wa upelelezi wa mkoa wa Dar es
Salaam hayakukata kiu ya itv kujua kama ni bomu au la hali iliyomfanya
kamanda Msangi pamoja na maafisa wa usalama wa taifa katika mkoa wa Dar
es Salaam kufanya kikao cha dharura ikiwemo kuperuzi katika mitandao na
kubaini kuwa kitu hicho huwa kinatumika katika masuala ya hali ya hewa
hasa kwenye viwanja vya ndege.Source ITV Newa- Tanzania