Rais
Kikwete ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano wa wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM Mjini Dodoma iliyokutana kama taasisi kujadili
maoni ya wanachama wake kuhusu mabadiliko ya katiba ambapo rais Kikwete
amesema katiba mpya ndio itakuwa dira ya maendeleo amani na ustawi wa
taifa kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Akimkaribisha
rais Kikwete kufungua mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Abdurahmani Kinana
amesema CCM imefanikiwa kukusanya maoni ya wanachama zaidi ya milioni
mbili na laki sita idadi ambayo mpaka sasa haijaweza kufikiwa na chama
chochote cha siasa.
Kabla
ya kufungua kikao hicho rais Kiwete alizindua Baraza la Ushauri la
Wazee la CCM ambalo litakuwa na majukumu ya kutoa ushauri kwa chama na
serikali katika mambo mbalimbali ambapo mwenyekiti wake ni rais mstaafu
wa awamu ya pili Mhe Alhaji Ali Hasan Mwinyi na katibu wake akiwa
makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM Mhe Pius Msekwa.Katika hatua nyingine
chama hicho kimetoa ufafanuzi kuhusu sakata la kufukuzwa kwa madiwani
nane huko Bukoba ambapo katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema
kamati kuu imeagiza Mweyekiti wa CCM na katibu wa Mkoa wa Kagera, mbunge
wa Bukoba, meya wa Manispaa ya Bukoba, pamoja mwenyekiti wa CCM Bukoba
mjini na katibu wake waitwe kujieleza mbele ya kamati kuu kuhusu sakata
hilo na baadaye kamati kuu itatoa maamuzi kuhusu sakata hilo.Kamati kuu
ya CCM na Halmashauri kuu ya chama hicho zinakutana mjini Dodoma
kujadili mambo mbalimbali huku ajenda kuu katika vikao hivyo ikiwa ni
kupitia maoni ya wanachama kuhusu mabadiliko ya katiba mpya na kisha
maoni hayo kuwasilishwa tume ya mabadiliko ya katiba ambapo ccm inatoa
maoni yake kama taasisi.source: ITV news-Tanzania