Monday, 28 October 2013

picha : Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani


Posted  Jumapili,Oktoba27  2013  saa 15:4 PM
Kwa ufupi
Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.


Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu, lakini ukweli utabaki palepale kwamba kitu au mtu hadi kuonekana mzuri, lazima kiwe kimekubalika na watu wengi.
Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani. Hiyo imesababishwa na umaarufu walionao walimbwende hao.
Lakini, umaarufu siyo kigezo cha kuwa mzuri kwani wapo watu wazuri mno na hawatambuliki, kwa sababu tu hawana umaarufu kama ilivyo kwa Angelina Joliea au Aishwarya Rai.
Miongoni mwa watu hao ni Fathima Zohar Godabari, raia wa Saudia Arabia, anayesadikiwa kuwa mwanamke mrembo kuliko wote walio duniani kwa sasa.
Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.
Mwonekano wa sura yake, urefu na wembamba wa wastani unatosha kudhihirisha mvuto wa hali ya juu alionao Fathima. Rangi ya ngozi, uzuri wa nywele na midomo yake inatosha kueleza na kukubali kuwa ndiye mrembo zaidi duniani kwa sasa.
Mrembo huyu anatoka katika familia ya kifalme ya nchini Saudi Arabia akitajwa pia kuwa mstari wa mbele kushiriki katika masuala yenye manufaa kwa wanawake.
Godabari pia ni mwanaharakati anayejihusisha na utetezi wa haki za wanawake na mshauri anayewakusanya wanawake katika makundi madogo madogo kwa lengo la kujisimamia na kupingana na aina yoyote ya ukatili dhidi yao.
Licha ya urembo na moyo wa kujitolea alionao, Godabari anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wanawake wachache kutoka nchi za kiarabu waliofanikiwa kupata kiwango cha juu cha elimu.
Kwa hivi sasa yuko nchini Uingereza ambapo anachukua shahada ya uzamili katika masomo ya uongozi wa biashara.
Historia kwa ufupi


Fathima Zohar Godabari alizaliwa Oktoba 22,1986 nchini India. Kwa sasa amefunga ndoa na Sheikh Awadi Al Muhammad wa ukoo wa kifalme nchini Saudia Arabia.
Imeandaliwa na Elizabeth Edward

SOURCE: MWANANCHI