Sunday 22 September 2013

Mugabe: “Fathers, we’re going to make it very, very tough for you. No molestation.”

Katika hali inayoonesha ni kukerwa na vitendo vya ubakaji na ulawiti, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameunga mkono maoni ya viongozi wa chama chake tawala cha ZANU-PF alipokuwa akiwahutubia kwa kusema kuwa kuwahasi wabakaji na walawiti ni mojawapo ya njia muafaka za kumaliza tatizo hilo alilosema limeenea sana nchini humo.

Vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya Zimbabwe vimenukuu Rais huyo siku ya Jumanne alipokuwa akihutubia viongozi na wageni wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Wizara ya nchi hiyo inayohusika na masuala ya ndani, shughuli za umma na makazi wakati wa kusherehekea Msimu wa Kwanza wa Bunge la Nane.

Amekaririwa akisema, “Vanababa tochenjera. Vaye movayambira, madzishe, vanobata twana tudiki, kana zvichinzi ndizvo zvinopedza hurwere, kana zvichinzi zvinopa mhanza here, kana upfumi, movaudza vazvikande pasi.  Fathers be aware. We
 are going to make it very, very tough for you. No molestation of youngsters, no molestation of women.

“We are going to increase ma-sentences. In the past there was death for rape, zvino vemahuman rights vanoramba hanzi ‘death haa no, it’s inhuman, it dehumanises a person,’ iye ari munhu atoita dehumanise vamwe. Kana wauraya munhu zvonzi a-ah, no, punishment of that nature is dehumanising, munhu akauraya mumwe? Ndipo pandinorambawo ipapa. Kungoti chete, if it comes in another way yekuti uyu akaparadza ropa toparadza rimwe here futi, so we have two people dying. An eye for an eye. Not in that way, ndaingoda for marapists kuti tisevenzise Burdizzo and the person remains alive. But that which makes him rape, must go. Kuna varume varikuramba ipapa” “We are going to increase sentences. In the past there was death for rape but these days those campaigning for human rights say its inhuman, it dehumanises a person. But these are people who dehumanise others. If you kill someone they say punishment of that nature is dehumanising, for a person who killed someone? This is where I disagree. An eye for an eye. Not in that way, I was thinking for rapists we should castrate them and the person remains alive. But that which makes him rape, must go. Are there any many here who are against that?” Alisema Rais Mugabe huku akishangiliwa na watu waliokuwa ukumbini wakimsikiliza.

Kwa mujibu wa takwimu za polisi nchini humo, zaidi ya watoto 1 600 waliripotiwa kubakwa na/au kulawitiwa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka nchini Zimbabwe.

Wabakaji wengi waliripotiwa kuwa ni ndugu, marafiki na jamaa wa karibu,  na wengi wao ni wale walioshauriwa na waganga wa kienyeji kuwa kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuponda maambukizi ya VVU/UKIMWI.

“Rape cases have increased by five percent as we recorded a total of 2,440 in the first half of the year compared to 2 326 recorded during the same period last year,” alisema hayo mwezi jana, msemaji wa Polisi, Superintendent Blessmore Chishaka na kuongeza, “We are concerned with this increase in rape cases because most of the case involved girls below the age of 16 years.”

Akitaja takwimu za wanawake, alisema kumekuwa na ongezeko la kutoka watu 773 hadi 812 waliobakwa nchini humo kwa kipindi kama hicho cha takwimu zilizoelezwa hapo juu.

Wanahistoria wamesema kuwa endapo Zimbabwe itatekeleza adhabu hii, haitakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani nchini Marekani, takriban miaka hamsini iliyopita walipitisha adhabu ya kuwahasi kwa kutumia kemikali wote waliothibitika kufanya ndono na watoto (pedophilics).

Nchini India nako, baada ya matukio mengi ya ubakaji kuripotiwa, baya zaidi likiwa lile la mwezi Desemba, Serikali ya nchi hiyo imepeleka muswada bungeni wa kutaka iweopo adhabu ya kutumia kemikali kuwahasi wabakaji ikiambatana na kifungo cha miaka 30.

Mwaka 2009 nchini Israeli, kaka ndugu wawili wanaoishi kwenye mji wa Haifa walikubali kuhasiwa kwa kutumia kemikali ili wajizuie wasifanye tena uhalifu wa wa kuwabaka watoto.

Nchini Australia, miaka mitatu iliyopita, mtu mmoja aliyekuwa na mazoea ya kuwabaka watoto aliponea chupuchupu kuhukumiwa adhabu ya kuhasiwa kwa kutumia kemikali, ila jopo la waliopitisha adhabu hiyo halikufahamu kuhusu matukio yake yaliyotangulia ya ubakaji.

Mwaka 2010, nchini Argentina katika mji wa Mendoza ilipitishwa sheria ya kuwaruhusu wabakaji wanaojitolea kuhasiwa kwa kutumia kemikali kama njia ya kimatibabu ya kuwasaidia wapunguziwe adhabu kwa makosa yao ya ubakaji.

Nchi nyingine zilizotajwa kuwa na sheria ya kuhasi wabakaji ni pamoja na Korea Kusini, Urusi na New Zealand.
 
SOURCE: WAVUTI.COM