Septemba 15, 2013
Raisi wa Zanzibar Ali Mohammed Shein siku ya Jumamosi (tarehe 14
Septemba) aliwataka wananchi kuisaidia polisi kuchunguza shambulio dhidi
ya mchungaji wa Kikatoliki Anselm Mwangamba ambaye alichomwa kwa
tindikali siku ya Ijumaa, shambulio la karibuni kabisa lililofanyika kwa
wanawake wawili wa Kiingereza mwezi uliopita, AFP iliripoti.
Mchungaji huyo mtu mzima aliunguzwa usoni, kifuani na viganjani, dakika chache baada ya kutoka katika kibanda cha intaneti huko Mji Mkongwe.
"Hatuwezi kuendelea zaidi kuishi kwa hofu na kuwa na watu wanaolengwa na majambazi kwa kutumia tindikali," Shein aliwaambia waandishi wa habari baada ya kumtembelea Mwangamba akiwa hospitali. "Mtandao huu wa kihalifu lazima utokomezwe, na watu wanapaswa kusaidia kumaliza tatizo hili."
Shein alitoa zawadi ya shilingi milioni 9.7 (dola 6,000) kwa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa wale waliohusika, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.
Kamisha wa polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa alisema kwamba mamlaka husika imewahoji baadhi ya washukiwa lakini bado hakuna ukamataji uliofanywa.
SOURCE: Sabahionline.com