Wengi
wa waliopata taarifa hii wanashangaa imekuwaje ni viungo vya binadamu
tu vimepatikana kwenye kontena vinaingizwa Kenya? Vilikuwa vinapelekwa
wapi? Kazi yake nini?
Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema shehena hii ilikamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa.
Inasemekana kuwa imesafirishwa na
mwanasiasa maarufu ambaye kabla ya kukamatwa alisema ilikuwa ni bidhaa
za nyumbani ambapo ilipofikishwa kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena
cha Changamwe na kupatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya
binadamu kisha amri ikatolewa ya kontena hilo kukamatwa.
Baadhi
ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na
mikono pamoja na bidhaa za nyumbani ambapo vyote kwa pamoja vilikuwa
vinasafirishwa.
Afisa
wa maswala ya uhusiano mwema wa KRA, Fatuma Yusuf alithibitisha kuwa
shehena hii iliingia kutoka China siku ya pili ya Oktoba 2013 kabla ya
kugundulika ilikuwa na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.
Mpaka
sasa uchunguzi wa shehena hiyo unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa
Mombasa wameonesha wasiwasi wao na kusema ipo haja ya serikali kutoa
ripoti ya ibada ya kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu
Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.
SOURCE: AZIMIO LETU