Mkazi wa mjini Songea, anadaiwa kujeruhiwa kwa mapanga na mtu anayedaiwa kuwa mumewe kisha kumuua shangazi wa mkewe.
Mwanamke huyo, Agatha Honde (19), ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mletele, eneo la Nonga Nonga, mjini humo, anadaiwa kucharangwa mapanga na mtu huyo.
Mtuhumiwa huyo inadaiwa kuwa baada ya kitendo hicho, alimuua shangazi wa Agatha kwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Agatha alisema anajisikia maumivu makali yanatokana na majeraha akidai yametokana na kukatwakatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa kwa sababu za kimapenzi.
Agatha alisema mwenza wake huyo kutokana na sababu zisizojulikana, aliamua kuachana naye na kwenda kuishi kwa shangazi yake.
Lakini akasema mtuhumiwa alimfuata na kumjeruhi kabla ya kumuua shangazi yake (55).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi, alisema baada ya mtuhumiwa huyo kufanya unyama huo, alikimbia na kwamba, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta popote alipo kwa hatua za kisheria.

CHANZO:
NIPASHE