Friday 11 October 2013

Waraka wa mashumbulizi wadaiwa kusambazwa


Na Mwinyi Sadallah

Posted  Ijumaa,Oktoba11  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Hata hivyo, alisema,tayari makachero wa Polisi wako kazini na ametoa wito kwa viongozi wa dini na wananchi kuondoa hofu kwa vile vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na tukio lolote la kihalifu.


Zanzibar. Waraka wenye vitisho ukiwa na nembo ya Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) umesambazwa visiwani hapa, ukidaiwa kutishia kufanyika kwa shambulio dhidi ya viongozi wa dini na Serikali kabla ya Sikukuu ya Eid El Haj.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kupata nakala ya waraka huo wenye maneno makali na vitisho kwa usalama wa watu na amani ya nchi. Kamanda Mkadam alisema,Polisi imefanikiwa kuupata waraka huo baada ya tukio hilo kuripotiwa na baadhi ya viongozi wa madhehebu za dini Visiwani humo.
Hata hivyo, alisema,tayari makachero wa Polisi wako kazini na ametoa wito kwa viongozi wa dini na wananchi kuondoa hofu kwa vile vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na tukio lolote la kihalifu.
Aliwahi wananchi kuendelea na jitihada za kuwafichua wahalifu na watu wanaowatilia shaka dhidi ya amani visiwani hapa.
“Hatua tulizochukua ni pamoja na kuwataka viongozi wa dini kuanzisha kamati za ulinzi mbali na kuwapatia huduma za ulinzi kama njia ya kukabiliana na matukio mbalimbali,”alisema Kamanda Mkadam.
Waraka huo unadaiwa kuainisha vitendo vya hujuma kuwa vitazidi hadi pale Zanzibar itakapofanikiwa kurejesha kile kilichoitwa Uhuru wake.

SOURCE: MWANANCHI