Monday, 23 September 2013

Bashir: 'Nitahudhuria mkutano wa UN, Marekani'


 23 Septemba, 2013 - Saa 05:56 GMT

Bashir anasakwa na ICC kwa tuhuma za uhalifu wa kivita
Rais wa Sudan Omar El bashir amethibitisha kwamba atahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New york juma hili, licha ya kusakwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Bashir anatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bashir amesema kuwa tayari amekodisha chumba cha kulala katika hoteli moja mjini humo na kwamba hatishiki kukamatwa na Marekani kwa kuwa sio mwanachama wa ICC.
Hata hivyo haijulikani iwapo atapewa viza kwa kuwa imekuwa utamaduni wa taifa hilo ambalo limetoa vibali hivyo kwa viongozi kama Robert Mugabe wa Zimbabwe na Mahmoud Ahmedinejad wa Iran kuhudhuria mkutano huo.

SOURCE: BBC SWAHILI