21 Septemba, 2013 - Saa 09:29 GMT
Wakuu wa Pakistan wanasema
wamemuachilia huru mfungwa mwenye cheo katika kundi la Taliban - Mullah
Abdul Ghani Baradar - ili kurahisisha juhudi za mapatano nchini
Afghanistan.
Serikali ya Afghanistan imekaribisha habari hizo
na inamuona Mullah Baradar kuwa mmoja kati ya maafisa waandamizi walio
tayari kuzungumza.Afisa mmoja wa Afghanistan alimuelezea Mullah Baradar - naibu kiongozi wa zamani wa Taliban - kuwa mjumbe wa amani.
Hata hivyo, waandishi wa habari wanasema haijulikani Mullah Baradar ana kauli gani bado katika kundi hilo la wapiganaji.
Alikamatwa mjini Karachi, Pakistan, mwaka wa 2010.
SOURCE: BBC SWAHILI