Na Habel Chidawali
Posted Jumatano,Septemba18 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumatano,Septemba18 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Ni wa Kampuni ya Italia ya SIETCO baada ya kulegalega katika ujenzi wa barabara ya lami huku akitoa visingizio.
Dodoma. Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
ameiagiza Kampuni ya SIETCO inayojenga Barabara ya Migori-Fufu, kuacha
visingizio na ikabidhi kazi hiyo Februari 15, 2014 kwa mujibu wa mkataba
vinginevyo ifungashe na kuondoka nchini.
Dk Magufuli alitoa agizo hilo jana, alipofanya
ziara ya kushtukiza katika ujenzi wa Barabara ya Dodoma–Iringa kwa
kiwango cha lami, ujenzi unaoendelea sasa.
SIETCO ni Kampuni ya Ujenzi kutoka Italia ambayo
ni miongoni mwa makandarasi watatu wanaojenga barabara hiyo yenye urefu
wa kilomita 260 kutoka Iringa hadi Dodoma na kipande chenye urefu wa
kilomita 93.8.
“Hawa watu hawafai kabisa, walivurunda kazi katika
Barabara ya Singida–Isuna hivyo wana rekodi mbaya na leo wanaonekana
kuwa watashindwa, sasa nawaagiza kuwa wakishindwa kukamilisha ujenzi huu
wasipewe kipande chochote cha barabara katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki,” alisema Magufuli.
Kuhusu kipande cha Barabara ya Dodoma-Fufu (Km
70.9), alimsifia Mkandarasi wa Kampuni ya China Communication
Construction Co. Ltd (CCCC), baada ya kujiridhisha kuwa ujenzi wake
umefikia asilimia 73.
Waziri Magufuli alisema, kumekuwa na tabia ya
baadhi ya makandarasi kugeuza Tanzania shamba la bibi ambalo kila mtu
anavuna na kuondoka.
Mhandisi wa ujenzi Mkoa wa Dodoma, Leonard
Chimagu, alisema ujenzi wa barabara katika mkoa huo unakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwamo ya wafugaji kutokutii sheria na hivyo
kupitisha mifugo kila wakati barabarani na kuharibu miundombinu.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI