Na Mwandishi wetu, Mwananchi
Posted Septemba7 2013 saa 11:57 AM
Posted Septemba7 2013 saa 11:57 AM
Kwa ufupi
Ofisa Biashara Mkuu wa Fast Jet, Richard Bodin,
alisema chini ya mkataba huo Watanzania wanaweza kusafirisha mizigo yao
ndani ya nchi kwa kutumia kampuni hiyo.
Dar es Salaam. Kampuni ya Ndege ya Fast Jet,
imeingia makubaliano na Kampuni ya kusafirisha mizigo ya Afrika ya
BidAir, kusafirisha mizigo kwa kutumia ndege.
Ofisa Biashara Mkuu wa Fast Jet, Richard Bodin,
alisema chini ya mkataba huo Watanzania wanaweza kusafirisha mizigo yao
ndani ya nchi kwa kutumia kampuni hiyo.
Alisema awali wateja wa Fast Jet Tanzania,
walikuwa hawana fursa ya kusafirisha mizigo mikubwa, lakini kwa sasa
wanaweza kufanya hivyo lakini kwa kupitia Kampuni ya BidAir.
source: Mwananchi
source: Mwananchi