Na Sharon Sauwa, Mwanachi
Posted Septemba7 2013 saa 11:55 AM
Posted Septemba7 2013 saa 11:55 AM
Kwa ufupi
Dodoma. Mgomo wa wafanyakazi wa Reli ya Tanzania
na Zambia (Tazara), uliodumu wa kwa wiki mbili, umesababisha hasara ya
zaidi ya Dola 14 milioni za Marekani.
Serikali imewataka tena wafanyakazi hao kurejea
kazini bila kukosa ifikapo Septemba 9 mwaka huu na kufanya kazi kwa
bidii ili kufidia hasara iliyotokana na mgomo huo.
Hayo yalisemwa bungeni jana na Waziri wa Uchukuzi,
Dk Harrison Mwakyembe, alipokuwa akiwasilisha kauli ya mawaziri kuhusu
mgomo wa wafanyakazi wa Tazara.
Kauli hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Spika,
Job Ndugai, alipokuwa akijibu mwongozo wa Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan
Kiwanga (Chadema) Jumatatu wiki hii.
Dk Mwakyembe alisema mgomo huo umesababisha treni 13 zenye mabehewa 252 ya mzigo kukwama njiani.
“Zaidi ya abiria 24,000 wenye tiketi wakimo watalii walikosa huduma ya usafiri wa treni.
“Wameshalipwa mishahara ya Mei mwaka huu na kuwa
ifikapo Jumatatu (Septemba 9 mwaka huu) watalipwa mishahara yao ya Juni,
Julai na Agosti.
Alisema Serikali mbili zimeagiza Bodi ya
Wakurugenzi wa Tazara kukutana mapema iwezekanavyo kwa ajili ya
maandalizi ya kikao cha Baraza la Mawaziri ndani ya Septemba mwaka huu .
Lengo la kikao hicho ni kutafakari ili hali iliyojitokeza na kuchukua hatua mara moja ili hali hiyo isijitokeze tena.
Mgomo huo ulianza Septemba 2 mwaka huu, uliitishwa
na Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), kudai malimbikizo ya
mishahara ya miezi minne.
source: Mwananchi
source: Mwananchi