Mkuu wa majeshi wa Kenya, Jenerali Julius Karangi amesema askari 11 walijeruhiwa na walikua wamelazwa katika hospitali ya jeshi, “Defence Forces Memorial Hospital.” Bahati mbaya kati ya majeruhi hao, watatu wamepoteza maisha.
Wengine nane bado wapo hospitalini hapo wakipigania maisha yao.
Taarifa kutoka kwa msemaji wa jeshi, Kanali Cyrus Oguna imesema kwamba KDF haitapungua ari katika jitihada za kumaliza operesheni katika jengo la Westgate Mall.
Utete na utata wa operesheni ya kuokoa mateka katika mashambulizi ya Westgate Mall yalihitaji uangalifu wa hali ya juu ili kuhakikisha usalama wa mateka. ” Canali Oguna amesema
Mkuu wa majeshi, Jenerali Karangi ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wanajeshi waliopoteza maisha yao na kuwasifia kuwa ni mashujaa walijitolea maisha yao ili kulinda nchi yao.