Katika
viwanja hivyo ulinzi uliimarishwa kutoka katika vikundi mbalimbali
vinavyomilikiwa na vyama hivyo huku shamra shamra za huko na kule
zikiwa hazikosekani ili mradi kunogesha mkutano.
Mwenyekiti
wa taifa wa Chadema na ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani
bungeni Mh Freeman Mbowe amewataka watanzania kuacha uoga na wasimame
imara kudai katiba bora.
Naye
mwenyekiti wa Cuf Mh Profesa Ibrahim Lipumba amesema Tanzani inahitaji
katiba ambayo italinda na kusimamia rasilimali za taifa kuweza kutmia
kwa usawa na kuzingatia mahitaji ya watanzania wenyewe.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mbuge wa kuteuliwa amesema
hakun haja ya kutumi mabavu na badala yake ameitaka serikali itumiye
busara zaidi ili kuweza kufiki mwafaka wa jambo hili.