Tuesday 3 September 2013

Makunga na wenzake kuanza kujitetea leo

Na James Magai  (email the author)

Posted  Jumatatu,Septemba2  2013  saa 20:46 PM
Kwa ufupi
Licha ya Makunga, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media inayomiliki gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na Mwandishi wa Makala katika safu ya Kalamu ya Mwigamba katika gazati hilo, Samson Mwigamba.

Dar es Salaam. Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, Theophil Makunga na wenzake wawili, wanaokabiliwa na kesi ya makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi, leo wanatarajiwa kuanza kujitetea.
Licha ya Makunga, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media inayomiliki gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na Mwandishi wa Makala katika safu ya Kalamu ya Mwigamba katika gazati hilo, Samson Mwigamba.
Washtakiwa hao wanatarajiwa kuanza kujitetea leo, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamua kuwa wana kesi ya kujibu na kuwataka wajiandae kwa utetezi.
Uamuzi huo ulitolewa Agosti 14, mwaka huu na Hakimu Mkazi Warialwande Lema, anayesikiliza kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka (Jamhuri) kufunga ushahidi wao.
Jamhuri ilifunga ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu; Mkurugenzi Msaidizi wa Usajili Magazeti, Raphael Hokororo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, George Mwambashi na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, David Hizza.

source: Mwananchi