Na Mwandishi Wetu
Posted Jumanne,Septemba17 2013 saa 2:0 AM
Posted Jumanne,Septemba17 2013 saa 2:0 AM
Kwa ufupi
Habari zinadai shehena hiyo ilisafirishwa kwa
kutumia pikipiki hadi Kituo cha Mabasi, lakini polisi tayari walikuwa
wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuhusu wizi huo.
Mara. Polisi wawili wa Musoma, Mkoa wa Mara na
Kibaha, Pwani wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha risasi
3,000 kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam.
Wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni aliyekuwa mtunza
chumba cha silaha Kikosi cha FFU Musoma na mwenzake mwenye cheo cha
Koplo Wilaya ya Kibaha, Pwani. Inadaiwa walikamatwa Juni 2, mwaka huu
saa 11:00 alfajiri.
Watuhumiwa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Musoma
na wamefunguliwa jalada MUS/RB/2465/013 wizi wa risasi 1,056, wanasubiri
taratibu zingine za polisi.
Habari zinadai shehena hiyo ilisafirishwa kwa
kutumia pikipiki hadi Kituo cha Mabasi, lakini polisi tayari walikuwa
wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuhusu wizi huo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo wahusika
wa basi na nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na stendi, baadhi
ya askari waliovaa kiraia walionekana maeneo hayo mapema.
Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka ndani ya
polisi, Koplo huyo alikutwa na shehena hiyo karibu na kituo cha mabasi
ya Kampuni ya Mohammed Trans, akijiandaa kuelekea Dar es Salaam ambako
inasemekana wana wateja wao.
Inadaiwa koplo huyo aliomba ruhusa ya ugonjwa
kazini kwake na kuitumia kusafiri hadi Musoma kuchukua mzigo huo,
inadaiwa biashara yao hiyo ni ya muda mrefu na wana mtandao na
watuwanaojihusisha na uhalifu.
Mtandao huo unadaiwa kuwagusa baadhi ya polisi
Mkoa wa Tarime na Rorya, ambao huwauzia watu wanaojihusisha na uhalifu
wa kutumia silaha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma alipotafutwa kwa simu zake za mkononi licha ya kuitwa, hazikupokewa.
Hata hivyo, aliomba atumiwe ujumbe, licha ya
kupelekewa huo ujumbe, hakujibu ingawa taarifa zinadai ameanza likizo ya
kustaafu hivi karibuni.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara, Jafari Mohammed
alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alikanusha kufahamu suala hilo huku
akigeuka kuwa mkali kwa mwandishi.
“Hilo mimi silijui, nani kakwambia wewe… askari
kukutwa na risasi mfukoni ni jambo la kawaida huenda ni uzembe
tunamshughulikia kwa uzembe,” alisema.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI