Na Mwandishi wetu
Posted Alhamisi,Septemba5 2013 saa 21:28 PM
Posted Alhamisi,Septemba5 2013 saa 21:28 PM
Kwa ufupi
Ni kweli tumefukuzwa kwenye kikao lakini
tunaomba ufumbuzi wa mgogoro wetu upatikiane kwa sababu haileti taswira
nzuri kwa viongozi kufukuzana kwenye vikao.
Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo
juzi aliwafukuza, Mkurugenzi na wakuu wote wa Idara za Halmashauri wa
Jiji la Arusha, katika kikao cha kujadili mfumo wa matokeo makubwa sasa.
Jana walitarajiwa kujadiliwa katika kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha.
Kikao hicho, kilifanyika juzi katika ukumbi namba
40 katika jengo la ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Arusha na kuwashirikisha
wakuu wa wilaya zote za mkoa huo, wakurugenzi na wakuu wa idara za
halmashauri.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho na ambazo
zilithibitisha na baadhi ya wakuu wa idara, zilisema mkuu wa mkoa
aliwafukuza kwa tuhuma za kukataa kutekeleza maagizo yake.
“Ni kweli tumefukuzwa kwenye kikao lakini tunaomba
ufumbuzi wa mgogoro wetu upatikiane kwa sababu haileti taswira nzuri
kwa viongozi kufukuzana kwenye vikao,”alisema mkuu mmoja wa idara ya
Jiji la Arusha.
Maagizo, ambayo yamemwingiza katika mgogoro
mkurugenzi wa jiji hilo ni kukataa, kuipa Kampuni ya Skytel, zabuni ya
kuendesha mradi wa taa za barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni,
mkurugenzi huyo Sipora Liana, alisema anataka taratibu za sheria ya
manunuzi ya umma zifuatwe .
source: Mwananchi
source: Mwananchi